الأدب السواحلي الإسلامي — الصفحة ٢٢٢

JAMIATUL - ISLAM (No. 15, ya 13 Ramadhan, 1349 H.) "JAMIA" katika lugha ya Ki-Arabu maana yake, ni kitu cha kuwafanyiza watu ni wamoja, wenye kusharikiana katika jambo maalamu. Watan mathalan, ni JAMIA wawataka watu wakaao katika mji mmoja wawe ni wenye kusharikiana katika maslaha ya mji wao, pasina tafauti baina ya kabila na kabila, wala baina dini na dini nyengine. Na JAMIATUL-ISLAM yawataka Waislamu wote ni kitu kimoja, katika kuivutia Dini yao mashala na kuiepushia madhara, kadhalika yamtaka killa Muislamu awe ni ndugu wa Muislamu Mwenziwe, pasina tafauti baina ya Muhindi na Mswahili, wala baina ya Muarabu na Mkikuyu, wala baina ya Mzungu na Mjawa, wala baina ya bora na duni, wala bwana na mtumishi wake. Mwenye-ezi-Mngu amewapangia Waislamu Wote UDUGU kwa neno lake alilosema kwamba “Waislamu ni ndugu" Na hikima ya ndugu huu, ni kutaka upatikane umoja wao, wasitangukane wakawa matapo mbali wala wasiwe killa taifa ni wakutetea nafsi zao tu, pasina kujali kuidhuru taifa nyengine. Kutangukana kwa watu ndiko kutakako ni mamoja, licho kuwa ni mbali na killa watu wapendelea nafsi zao tu. Tazameni majeshi ya Islamu yaliyo kwenda kufutahi miji ya Sham zamani za Sayyidina Abubakar, yalikuwa ni matapo mane: Amru bin El-as na tapo lake na Abu-Ubaida na tapo lake, Yazid bin Abi-Sufyan na tapo lake na Shar habil bin Hasana na tapo lake. Na wote hao hapana shaka yakuwa makusudio yao yalikuwa mamoja na kupendana kwao ni kama tujuavyo, lakini kwa sababu ya kufarikana, hawakuweza kawashinda Warum, hatta alipokwenda Khalid bin El-Walid akayakusanya matapo yote mane akayafanya ni jeshi moja tini ya uamrii wake, ndipo walipo shinda maadui. -۲۲۲ -
ص ٢٢٢

النص مستخرج آليًّا من صور الكتاب، وقد يقع فيه خطأ.