الأدب السواحلي الإسلامي — الصفحة ٢٠٥

Hata hivyo vituko vya aina hii viliendelea mpaka mwisho wa safari yake Johari. Basi Johari alipofika mjini Istiska aliimba kwa sauti nyororo: Nisafiri upesi upesi, Nifike haraka haraka. Baba amenituma mvua. Amenituma mvua kwa Mirambo, Nani atamionyesha kwa Mirambo? Mara bibi mrembo alitokea akanena, ‘Njoo hapa mwanagu: nami nitakuonyesha. Nenda hadi kwenye nyumba iliyoko mkono wa kushoto. Hapo ndipo anapoishi Mirambo.' Johari aliifikia nyumba ile lakini hakumkuta Mirambo, bali alionana na mwanae aliyeitwa Isike. Baada ya Johari kueleza aliyotumwa, Isike alimwonyesha nyumba ya yule Mkwawa, mganga mahiri aliyeshika mvua. Lakini kabla ya kuondoka Isike alimweleza Johari haya, "Chukua huyu nyuki na nenda naye mpaka kwenye nyumba hiyo ya mganga Mkwawa. U rafiki usikubali kukaa viti vyake kwani ni vichafu. Ukipewa chakula dai wakutilie katika chombo safi na kisha omba maji ya kuoga. Baada ya kuoga watakuambia kuchagua mkoba. Kabla ya kufanya hivyo ni lazima umrushe huyu nyuki na mkoba atakaotulia ndio utakaouchukua. Usifungue wala kuondoka kabla ya mwenzako kuwasili”. Johari akaenda mpaka kule. Alipofika alitendewa yote kama alivyomwambia. Hata alipoambiwa kuchagua mkoba, alimrusha nyuki wake ambaye alitua kwenye mkoba safi kabisa. Johari alikuwa na furaha isiyo na kifani. Huku nyuma Majonzi amekuwa akikutana na viumbe vya ajabu. Lakini kwa moyo wake mkunjufu amevisaidia. Wenye vidonda amewasafisha, maskini amewaondoa barabarani na vipofu wote wamewachecheza njia. - ٢٠٥ -
ص ٢٠٥

النص مستخرج آليًّا من صور الكتاب، وقد يقع فيه خطأ.